Ni Lazaro Nyalandu tena Singida Kaskazini

Lazaro Nyalandu amefanikiwa kukitetea kiti chake kama Mbunge wa Singida Kaskazini baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu. Chama Cha Mapinduzi kimeshinda kata zote 21.

IMG_0213

Mbunge mteule wa jimbo la Singida kaskazini, Lazaro Samwel Nyalandu (katikati) akiwa amepumzika akisubiri kutangazwa kwa matokeo ya nafasi ya ubunge leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida vijijini, Naruba Hanje na kulia ni Shyrose Matembe anayewania nafasi ya ubunge viti maalum mkoa wa Singida.
IMG_0239
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida kaskazini, Hajat Farida Mwasumilwe, akimkabidhi cheti cha kuthibitishwa kuwa mbunge, Lazaro Samwel Nyalandu leo.
IMG_0249
Mbunge mteule Lazaro Samwel Nyalandu, akiwa mwenye furaha kubwa baada ya kutangazwa kuwa mbunge jimbo la Singida kaskazini jana. Wa kwanza kushoto ni msaidizi wa mbunge mteule Nyalandu, Elia Digha ambaye pia ni diwani mteule wa kata ya Msange jimbo la Singida kaskazini.
 
IMG_0204
 
Mbunge mteule wa jimbo la Singida kaskazini kupitia tiketi ya CCM, Lazaro Samwel Nyalandu, akisalimiana kwa furaha na Mwandishi wa habari wa Azam TV mkoani Singida, Doris Meghji kwenye viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini leo muda mfupi kabla ya kutangazwa kushinda nafasi hiyo kwa awamu ya tatu mfululizo.
 
IMG_0254
Mbunge mteule wa jimbo la Singida kaskazini,(katikati mwenye fulana ya bluu) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutangazwa kutetea vema nafasi yake hiyo.(Picha na Nathaniel Limu).

IMG_0258